Wednesday, November 11, 2015

Arusha Reader's Club for you and your little one




Hii ni habari njema sana kwako wewe mzazi na mtoto uliyeko Arusha.

Kwenye post zangu za nyuma niliongea kuhusu umuhimu wa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu. Sasa Arusha kumeanzishwa club inayoitwa Arusha Readers' Club. Hii ni mahususi kwa wazazi ila na watoto pia.

Unajiungaje?
Unaweza kujiunga na Arusha Readers Club ARC kwa ada ya Uanachama kwa mwaka mzima ni Tsh 50,000 (elfu hamsini tu) na unaweza kulipa kwa awamu mbili.

Watoto wa umri gani wanaruhusiwa?
Klabu ya watoto (Kids Club) inaruhusu watoto wa umri wa miaka 3 hadi 7. Watakutana na mwandishi wa vitabu vya watoto (vya Kiswahili na Kiingereza)Honorina Mashingia ambaye  atawasomea hadithi kutoka katika vitabu hivi

Wapi na saa ngapi?
Bustani ya MWEDO Coffee Shop kuanzia (saa tatu (3) hadi saa tano (5) asubuhi). 
MWEDO coffee shop iko barabara ya Phillips baada ya Impala Hotel na KK Security

Mawasiliano?
Kwa maelezo zaidi wasiliana na viongozi waandamizi wa ARC Anna Ndiko Emmer Saitoti Redy MartinPaul Saing'eu au piga simu zifuatazo 0762563276, 0654335728, 0762355392

Until next time, usisahau kujiunga na unaweza kuwa "Like" on facebook Arusha Reader's Club au follow the link https://www.facebook.com/970241966373380/photos/pcb.983709058360004/983708265026750/?type=3&theater

"We Love Books"
ATM

No comments: