Thursday, May 26, 2016

Agape's 5km Marathon

Habari za siku nyingi,

Naamini muwazima na mmeshapata nakala zenu za video ya War Room.

Image result for life is like a marathon
Wiki iliyopita nilipata bahati ya kushiriki marathon moja hivi na nikakimbia kilometa 5. Nilipoenda kama mita 200 nilikuwa nimechoka sikuwa na viatu sahihi vya kukimbilia,niliamua nitatembea badala ya kukimbia tu. Baba mmoja ambaye naye alishiriki alikuwa amechoka ila aliniambia mama twende. Kila akitangulia mbele yangu kidogo aliniambia jitahidi, twende etc. Na kila akisema hivi naongeza mbio au mwendo alifanya hivi mpaka nilipomaliza
Image result for life is like a marathon

Mbio zilifanyika barabarani kwa hiyo palikuwa na watu wanaoangalia. Kuna walioamua kunicheka tu bila sababu,wengine waliniambia kimbia dada unaweza tu. Wengine waliniambia siwezi chochote niache tu. Wengine walinitukana. Wengine waliniambie nipande baiskeli zao na pikipiki mpaka daladala. Wakati nakaribia kumaliza mbio mtu mmoja aliniambia wewe kwanza hata hujakimbia, ulikuwa umekaa tu mahali umejificha ndo umetoka ili umalize. Wewe huwezi kitu.

Wakati wa mbio mara nyingi nilitamani kuacha ila huyu baba ambaye na yeye alikuwa kwenye mbio hakuruhusu aliendelea tu kuniambia twende, fanya bidii. Usiache. Wakati wa mbio niligundua kuwa huyu baba hakuangalia nyuma kabisa, he kept going and looking forward, he was tired but he went and looked forward. Aliniambia, "Nawaangalia wale walioko mbele yetu, karibu tunawafikia". I doubted maneno yake ila we kept going.


Image result for life is like a marathon
Hii ilinifundisha somo kubwa sana kuhusu maisha. Life is like this marathon. Unafanya jambo ila kuna mambo mengi yapo njiani. Utakutana na watu wa aina nyingi kama hawa ambao nilikutana nao mimi. Wengine watakupa moyo, wengine watakukatisha tamaa wengine watakucheka, wengine watakutukana na kukudhihaki.

Cha muhimu kabisa ni PUT ON THE RIGHT SHOES, songa mbele. Never look back, look those who are before you. You went through a bad life experience, never look back look forward. In life keep moving, it does not matter how you move. Run, walk,crawl, just move. Mambo yanaweza kuwa magumu hakuna kukata tamaa, hairuhusiwi kukata tamaa, hakikisha unamaliza what you started.

Hata kwenye malezi ni hivyo hivyo. Kumbuka wewe ni mama au baba bora. Tia bidii. Omba, fanya kila kinachowezekana kufanyika kulea watoto vizuri. Hakuna mzazi perfect duniani. Tunakosea ila tunasahihisha tunasonga mbele tu.

Run your marathon well.
Image result for life is like a marathon

With love,
ATM