Wednesday, August 12, 2015

Njia sahihi za kumlea mtoto katika picha: How to handle the baby, illustrated

Habari,

Naamini muwazima, mimi pia. Nimepita kwenye mtandao nikaona picha za jinsi ya kuhandle watoto, nimeona ni vema kukushirikisha.

Usisahau kumshirikisha mwingine


Source:

http://archiengineering.com/who-have-no-clue-what-to-do-with-a-baby?pageno=30

Haya nikutakie malezi mema.

ATM

Monday, August 3, 2015

For the love of fashion: Meet Zoe Glorious

Habari,

Naamini wewe ni mzima. Samahani kwa kuwa kimya sana, ila mambo yote ni mema. 

Kwa kipindi cha kama miezi miwili nitaweka posts za watu ambao ni ordinary na wanafanya mambo mazuri na wana-inspire wengi. 

Leo naanza na Zoe Prudence Shoo


Image result for zoe malaika glorious
Nimemfahamu Zoe nikiwa Shinyanga Commercial Institute. Siku ya kwanza nimefika shule (Tulikutana bafuni....hahahaha).  Ndani ya dakika chache urafiki ulizaliwa.

Nilisema mimi napenda fashion ila Zoe ni fashion Icon, yaani akiwa mbele ya kioo is all fashion. Watu waliosoma Shycom wanaweza kukueleza jinsi Zoe alikuwa anapenda sana kupiga picha and she had her heart in all the pictures she took. Sisi tuliona ni ordinary pictures ila kwake it was a way of making her identity. 

A fashion Icon.

Nilipomuuliza Zoe aniambie kuhusu yeye kwa kifupi aliniambia yeye ni Creative, Zoe has the ability to think outside the box na kukupa jambo la tofauti, haogopi kuthubutu na hilo ni jambo ambalo linamfanya yeye kuwa mtu wa tofauti sana na kati ya watu ambao ningependa kufanya naye kazi huko baadae ni yeye.

Nilipokuwa nawaza kuhusu Creativity ya Zoe niliwaza kuwa ili Zoe aweze kuwa mtu creative ilihitaji kuwa na wazazi waelewa. Nimepata bahati ya kukutana na mama yake na nilijua kwanini Zoe ni mtu wa tofauti sana.
Image result for zoe malaika glorious 
Wazazi tuna nafasi ya muhimu sana ya jinsi watoto wetu wanavyoweza kuja kuwa wanapokuwa watu wazima. Naamini kwenye kumruhusu mtoto kuwa na imagination na kumtia moyo na sio kumkataza kila  jambo, tunawawekea vikwazo katika kubuni mambo kwenye maisha. Mtoto wangu ana potty ambayo inakuwa assembled upya kila anapoitumia…alipoanza kutumia tulimpa nafasi ya kurudisha potty katika hali yake ya mwanzo na ni jambo analo weza sana.

Jambo lingine ni kumruhusu kutumia vyombo vyote, hata vinavyopasuka. Genesis hajafikisha miaka miwili ila anajua kuwa chombo hiki ni delicate na kina hitaji extra care na kwa jinsi hiyo anakuwa na confidence. Haya ni mambo madogo ila yanaweza kuleta impact kubwa kwa mtoto

Zoe ni mtu ambaye ana huruma na upendo wa ajabu, ni kati ya watu jasiri sana niliowahi kukutana nao. Ni mtu mwenye sincere heart na nimekwambia hapo juu kuwa nilipokutana na mama yake nilijua kwanini. Jinsi tunavyowapenda watoto wetu na kuwalinda inawapa confidence katika jamii ila pia inawasaidia kuwapa watu wengine the same amount of love they have received from us. Wapende watoto wako sana it can change the world.
Image result for zoe malaika glorious
Jambo la muhimu sana la mwisho ni kuwa Zoe ana interest sana na kusoma vitabu. Hii hobby ameniambukiza kidogo pia na inampa sana upeo wa kufanya vitu vingi hata creativity yake vitabu vimekuwa na nafasi kubwa sana. Hili swala la kusoma vitabu nitalileta kwenu kwa undani

Asante sana Zoe kwa kuniruhusu kueleza KUHUSU wewe. Kwako sky is the limit....Naamini nitaandika tena kuhusu wewe siku nyingine.

Stay tuned for more
Image result for zoe malaika glorious

ATM