Tuesday, November 24, 2015

Baby Blues: Huzuni baada ya kupata mtoto

Habari wapenzi wasomaji..

Naamini muwazima. Hii mada inaweza kuonekana ni ya utata ila ni ukweli. Kama haijakutokea wewe imemtokea yule.

Kwa wengi wetu swala la mtoto ni furaha na huwazi kama kunaweza kukawa na depressions...na wazungu waimeita hii hali "Baby Blues". Ila ikiwa zaidi inaitwa Postnatal Depression (PND).

Image result for baby blues
Hali hii ya "baby blues" inawatokea wanawake 8 kati ya 10 ya wanaopata mtoto. Hali hii inakuaje?


  • Unakuwa na mashaka kuhusu hali ya mtoto hata kama mtoto ni mzima wa afya
  • Kuwa na hali ya wasiwasi kila wakati (Anxiety)
  • Kuwa na hali ya kukosa umakini (Unable to concentrate)
  • Unasikia kuchoka na unashindwa kulala
  • Kulia bila sababu
Image result for baby blues
Je inasababishwa na nini?
  • Mabadiliko ya homoni kwenye mwili hasa ile wiki ya kujifungua hasa homoni ya adrenaline
  • Hisia za wajibu wa kuwa mzazi nazo zinaweza kusababisha hali hii
  • Unapotoka hospitali na unapogundua kuwa kweli sasa umekuwa mzazi na majukumu ni yako hii inaweza kuzidi hasa unapokuwa single parent..na hii inaweza kusababisha hali hii
  • Kutokujua jinsi ya kumlea mtoto wako inaweza kusababisha hali hii. Unapochoka sana na hupati usingizi na kuchoka kwa sababu pia huna msaidizi inaweza kusababisha hali hii
Je hali hii inakaa kwa muda gani?

Huu si ugonjwa na hivyo kutokana na mazingira inaweza kuwepo kwa masaa au siku kadhaa. Ukipata mapumziko ya kutosha na msaada kutoka kwa familia na ukipata mtu wa kukutia moyo basi hali hii huisha yenyewe bila kumuona daktari

Ila hali hii ikiendelea kwa miezi ni vyema kumuona daktari inawezekana una depression ya baada ya uzazi

Je nawezaje kumsaidia mtu mwenye hali hii?
  1. Msaidie kupanga timetable ya kipi kifanyike kipi kiachwe
  2. Msaidie kuandaa chakula 
  3. Mtie moyo apumzike sana
  4. Mueleze kuwa yeye ni mama mzuri
  5. Punguza wageni wanaomuona
  6. Akitaka kulia muache alie
  7. Msikilize.
  8. Usimwambie asilie mbele ya mtoto ajikaze tu maana ndo ukubwa. Hii haimsaidii inamfanya azidi kujiona ni mama mbaya na inaongeza hali kuwa mbaya
Image result for baby blues
Je kama ni mimi nifanyeje?

Hali hii ilinitokea na nikwambie ukweli si rahisi.

  1. Omba, mwambie Mungu akusaidie uweze kulea mtoto vizuri na aondoe hiyo hali, yeye ndo amekuumba anaijua hiyo hali
  2. Omba mtu akusaidie kukaa na mtoto unapojisikia unahali hii ili upumzike na ulie vizuri
  3. Lia, kama unataka kulia lia sana
  4. Sema unavyojisikia, usiweke mambo ndani
  5. Badili activities pale unapojisikia vibaya fanya kitu unachopenda...mimi ilikuwa kuangalia movie.
You can search this topic on the internet and learn more

Image result for baby blues
Until next time, remember, YOU ARE A GREAT MOM
ATM

No comments: