Monday, June 27, 2016

ME TOO: MIMI PIA

Habari wapenzi wasomaji,

Naamini wote muwazima wa afya. Nimemiss kuwepo kwenye screen yako, na namshukuru Mungu kwa nafasi hii.

Image result for me too
Wengi wetu wakati tukiwa wadogo tulikuwa tukisikia wazazi ambavyo kila jambo unalofanya anakwambia yeye hakuwahi kufanya akiwa mdogo. Na kila mzazi alikuwa anakuwa wa kwanza shuleni. Ni watu wachache sana walioambia watoto wao kuwa shuleni alikuwa mtundu, mchokozi, alichapwa sana na alikuwa hafanyi vizuri sana darasani.

Hii haimaanishi kuwa wazazi wetu walikuwa wazazi wabaya, la, ilikuwa ni njia yao waliyoamini kuwa itatusaidia kuwa inspired kuwa kama wao. Ukweli ni kuwa njia hii si sahihi. Kwa sababu mtoto anaishi kwenye uongo na akijaribu sana kukufurahisha na kujiona ni mtu asiyeweza na kushangaa inakuwaje yeye ni mtoto wako na anafanya vibaya darasani au anaishia kukosa kila siku.

Image result for me tooHii inamjengea mtoto kutojiamini na kuwa mnyonge sana. Na pale atakapokuja kujua ukweli kuwa haukuwa kama ulivyomueleza, mara nyingi inamsababishia kutokukuamini tena na kuamua kuwa huru kufanya anavyojisikia.

Hii si kwa wazazi tu, ni jambo liko kwenye jamii, wahubiri na wachungaji, viongozi wa dini na makampuni hawapendi kuwaeleza watu "Failures" zao au mapungufu waliyokuwa nayo na jinsi walivyo yashinda na hii inatufanya kuwaona watakatifu na kujaribu kwa nguvu sana kuwa kama wao na saa ingine inatusababisha kujiona wabaya tusio na bahati, wajinga na wenye hasara sana.

Muhubiri mmoja alisema kuwa anapenda sana kumtumia mfalme Daudi anapowahubiria wanaume, Daudi ni mfano mzuri wa mambo wanaume wengi wanapitia na inakupa moyo kuona kuwa Mungu anasemehe na anakufanya mkuu.

Image result for me too
Kama wazazi ni vyema kuwa na tabia ya kushare challenges zako ulizopitia na mafundisho uliyopata ili kizazi chetu kipone. Tuwe wazazi wanaosema "ME TOO". Mfanye mtoto wako ajue ulivyo.

Do you struggle to be a perfect parent?- ME TOO
Do you feel you are not doing good enough for your children- ME TOO

I wish you a great week,
We are in this together
Image result for me too
Love,
ATM