Friday, October 30, 2015

Wajifunze kujiamini: Teach them to be confident

Habari wasomaji wangu,

Poleni na hongereni kwa mikiki mikiki ya uchaguzi.

Leo tuendelee na zile tips tulizoanza nazo wiki iliyopita:

Image result for raising a confident child
4. Praise them on small accomplishments. Mtoto anapofanya jambo jema hata liwe kidogo kiasi gani mtie moyo kwa kumpongeza, hii itampa hari ya kujaribu tena na tena

5. Allow them to choose their own path. Hii najua ni ngumu kuelewa ila ni muhimu kumzoesha mtoto kuchagua wenyewe njia wanayotaka kupita kwenye maisha. Tangu anapokuwa na kama miaka miwili mruhusu aamue nguo ya kuvaa n.k. Baba yetu hajawahi kutulazimisha kuwa watu fulani, amekuwa guardian tu, anaonyesha options tulizonazo na kuturuhusu kuamua

Image result for raising a confident child6. Ongea nao kuhusu strength zao na weakness zao. Hii itawasaidia kujua kuwa wana uwezo gani na wafanye bidii ya kuongeza yapi na kujifunza nini zaidi. Hii pia inasaidia watoto kuamua hata career (Kazi) zao za badae

7. Trust them. Jifunze kuwaamini watoto hata kama unapata shida kiasi gani. Wewe ndo mtu wa kwanza kuona jambo lao lolote na hivyo wanatamani uwaamini kuwa wataweza. Waruhusu kubeba glass na kadhalika


8. Have their back at all times, protect your own. Mimi huwa nashangaa mzazi anayeitwa shuleni na anasema, "Kweli huyu mtoto mjinga sana, hata nyumbani ni mzembe sana". Hii si sahihi, watoto wako wanategemea uwe upande wao, hata wanapokosea waonyeshe upendo na kuwasahihisha kwa upendo. Baba yangu na mama wamenichapa sana ila kila wakati najua wanaangalia my interest na hawawezi kuwa upande wa mtu mwingine zaidi yetu.

9.Allow them to be them not to be who you could not be. Baba yangu ni mwalimu, engineer na mama ni mwalimu ila hawajawahi kutushawishi kuwa wao, wametaka tuwe vile tunaona tunataka tuwe. Na tumefanya hivyo.

10. Give them a chance: Wape watoto nafasi ya kufanya mambo usitake kufanya kila kitu usiweke dada wa kazi wa kufanya kila kitu. Wape nafasi ya kujifunza kujitegemea


11. Give them constructive criticism. Jamani hii si kwa watoto tu ila hata kwetu. Inaumiza sana mtu anapokukosoa vibaya, ni vizuri kutumia nafasi hiyo kumweleza kuwa ni kwa jinsi gani angefanya vizuri zaidi. Nilipoingia form 1 nilikuwa wa 41 darasani kati ya watu 96, nikiwa shule ya msingi nilifeli mara moja nikawa wa tano (5), niliogopa sana. Ila baba aliniambia, " Agape ukijua kingereza vizuri utafanya vizuri sana".
Image result for raising a confident child
12. Learn to say SORRY. Najua kiafrika hii inakuwa nguvu, tunajiona kama vile sisi ni miungu na hatukosei watoto wetu. Ila sisi pia ni wanadamu na tunawakosea. Unapomuomba samahani anaona kuwa hata yeye anastahili heshima na ni mtu wa muhimu. Na hii itampa sana ujasiri na atajifunza kufanya hivyo kwa wengine.

13. Be their example of confidence: Jamani sisi ndo kioo cha watoto wetu, hawawezi kujifunza kama hawataona kwetu. Jiamini wewe na yeye itakuja kirahisi.

14. Show them that they are important by spending time with them. Jamani watoto wanaoingia kwenye makundi mabovu huwa hayo makundi yanawaonyesha kuwa wao ni wa muhimu na hivyo wanawabadili. Mpe mtoto muda wako aone yeye ni wa thamani sana na hii itamsaidia asisumbuliwe na mtu yeyote. Anajua anaye anayemthamini nyumbani.

All the best.
Image result for raising a confident child

ATM

No comments: