Wednesday, July 13, 2016

Jinsi sahihi ya kumlaza mtoto mchanga: Laying down your new born

Habari wapenzi wasomaji wangu.

Image result for how to lay down a newborn babyNaamini wote muwazima na mnaendelea vyema na shughuli zenu.

Mara nying tumekuwa tukisikia mtaani kuwa ukitaka mtoto alale vizuri mlaze kwa TUMBO. Hii imeaminiwa na watu wengi sana.

Mtoto mchanga HAPASWI kulazwa kwa tumbo wala kutumia mito. Mlaze mtoto kwa MGONGO. Hii inapunguza uwezekano wa mtoto kusuffocate (kukosa hewa).

"The American Academy of Pediatrics recommends that healthy infants be placed on their backs for sleep, as this is the safest position for an infant to sleep"

Mara nyingi tunasikia mtoto alikufa ghafla usingizini na tunabaki kushangaa kwanini. Mtoto mchanga ni rahisi sana kukosa hewa tofauti na mtu mzima. Akikosa hewa kidogo tu basi amefariki.
Image result for how to lay down a newborn babyJinsi ya kumsaidia mtoto kupata usingizi haraka:

  1. Hakikisha mtoto amekula akashiba
  2. Hakikisha ni mkavu, mbadili nepi kabla ya kulala
  3. Hakikisha mtoto amecheua. Hii inaondoa gesi tumboni inayosababisha mtoto kuumwa na tumbo. Baada ya kula kuwa na muda wa kutosha kumcheulisha mtoto.
  4. Wakati unambembeleza muimbie taratibu alale
  5. Ondoa vitu ambavyo vinaweza kumkosesha hewa mtoto kitandani. Mfunge vizuri na blanket au baby shawl. Weka midoli mbali na mtoto akiwa amelala
  6. Unaweza kumfanyia massage tumboni na miguuni taratibu akiwa analala
  7. Hakikisha mtoto hafunikwi sana akapata sana joto au akaachwa kufunikwa akasikia baridi
  8. Tumia muda wa mchana mwingi kucheza na mtoto ili alale zaidi usiku 
Unaweza soma zaidi mtandaoni

Wishing you happy parenting.
Yours,
ATM