Friday, March 18, 2016

Endometriosis, A silent struggle just got a voice

Have you ever had to write something with a lot a lot of emotions that you are shaken? Well this is me and I will tell you I will take up to 3 days to write this maana I need to compose myself to put this well.

Karibu.
Image result for millen magese endometriosis

Ok i have postponed this post kwa muda sasa ila ni wakati muafaka kuiweka. Nisameheni nitachanganya lugha sana

Endometriosis ni nini?
Ni hali inayotokea pale tishu zinazotakiwa kuota ndani ya kizazi (Endometrium) zinaota nje ya kizani na kuasababisha maumivu makali sana. Maumivu haya hutokea wakati wa hedhi, baada ya kufanya tendo la ndoa etc.

Ni nini dalili za Endometriosis?

  • Maumivu MAKALI kabla na wakati wa hedhi.
  • Maumivu sugu kwenye tumbo la chini na gongoni kwa chini
  • Maumivu wakati na baada ya tendo la ndoa
  • Kuona damu katikati ya mwezi kabla ya siku ya hedhi na kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi
  • Inasababisha pia kupata maumivu makali wakati wa kupata haja kubwa na ndogo
  • Baadhi ya watu wanakua na maumivu kiasi na wengine hushindwa kabisa kufanya kazi zao za kila siku.
  • Kushindwa kupata mtoto na wakati mwingine kunakuwa hakuna dalili kabisa

* Kuna watu wasiopata dalili kabisa

Nani anaweza kupata Endometriosis?
Mwanamke yeyote anaweza kupata Endometriosis, ila watu wengi wanajua hali yao wakiwa na miaka kama 30-40 hivi. Na uko kwenye hatari zaidi ya kupata shida hii kama, Hujawahi kupata mtoto, Hedhi yako hukaa kwa siku 7 au zaidi.
Image result for millen magese endometriosis
Utajuaje kuwa una Endometriosis?
Nenda hospital onana na daktari. Atakuuliza maswali kuhusiana na dalili na kucheck kama una makovu kwenye kizazi, "pelvic" na "cysts" . Wanaweza kukufanyia MRI au kukufanyia kitu kinaitwa "Laparoscopy", hiki kipimo kinafanyika kwa kuingiza kameraa kwenye tumbo kwa kufanya upasuaji mdogo, hii itaonyesha kama kuna vioteo vyovyote kwenye tumbo.

Je Endometriosis ina tiba?
Endometriosis haina tiba. Kama dalili ulizonazo si kali sana basi dawa za kutuliza maumivu zinatosha. Saa ingine doctor anaweza kukupa dawa za kusaidia homoni zako. Dawa zaweza kuwa za uzazi wa mpango ila hazitumiki kama unataka kupata mtoto baada ya muda mfupi.
Kama una maumivu makali sana basi inabidi operesheni ili kuondoa vimelea, vimelea hivi wakati mwingine hurudi pia. Kwa watu wengine ambao imekuwa kali sana basi hufikia hatua ya kutoa kizazi.

Kwanini nimeweka hii post wakati huu?
Pamoja na kushusha uwezo wa kufanya kazi kwa usanifu kwa wanawake wengi duniani kwa kuwasababisha walale vitandani na kushusha uchumi wao na familia Endometriosis inasababisha ugumba. Na hii kwa jamii zetu inasababisha maumivu sana kwa wanawake na kuvunjika kwa ndoa nyingi.

 Wengi tunamfahamu Millen Magese zamani alijulikana kama Happiness Magese. Huyu alikuwa Miss Tanzania na sasa ni mwana mitindo wa kimataifa. Yeye anaEndometriosis na ameamua kusema na kuwasaidia wasichana wengine walioko mashuleni ili wajue athari za hii hali.

Mwezi March ni mwezi wa kutoa habari "Awareness Month" ya Endometriosis. Ni muhimu sisi kama jamii kujua swala hili na kuwasaidia dada zetu, rafiki, mama,shangazi, wake zetu na watoto wetu wanaokua.

Kwa miaka mingi imekuwa ni aibu kwa wasichana kuongea mambo yao ya siri hadharani ila sasa inabidi liongelewe ili tupone. Na pia jamii iache mila potofu kuwa maumivu ni sawa tu, hapana, ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya zetu. Jamani tusiende tu hospitali mambo yakiwa very serios, tukiwahi hospitali msaada unaweza kutolewa na kuzuia athari zaidi.

This post is dedicated exclusively to Millen Magese, who fights Endometriosis on daily basis and who maintains a positive attitude and inspires million of people around the globe.

Asante sana dada Millen.

Unaweza kumfollow Millen Magese na Foundation yake kwa kufuata below links

Ladivamillen, MillenMageseFoundationEndometriosisAfrica, EndometriosisSwahili. Unaweza pata habari nyingi kuhusu Endometriosis kwenye Google.

Tazama video iliyotengenezwa na BBC wakati wa kampeni yake ya Africa Unsung Heroes iliyoonyesha clip ya Millen Magese. Bonyeza hapa

With Love,
ATM.

Monday, March 14, 2016

Happy New Year 2016

I know it is silly to say Happy New Year at this time of the year but well, it is still a young year right na sikuwapa pongezi za kuona mwaka. So Happy New Year to my lovely readers.

I believe mwaka umeanza salama na mipango yako inaenda vizuri, if not yet, be patient and work hard, keep going they will happen in due time.

When the year was ending I said about resolutions and just keep them somewhere, I have never real see all of them through ila I keep working as hard as possible. Please usikate tamaa, keep pushing you will get there.

I have a good feeling about this year, I believe that it is called HOPE and I have seen that a lot of people are being positive too and so I do wish that you get positive, PRAY so MUCH and WORK hard.

Remember to keep family goals in check but usisahau PERSONAL goals. When one is happy and satisfied with their circumstances and they get a sense of accomplishment, They tend to work better and help others better to achieve their goals. A happy soul affects others positively.

I have been lazy posting here that is because......
well I am putting in check some of those resolutions I have suspended for long, hahahaha, ila sit tight a lot is coming.

I wish you and your family a wonderful new year and may success and happiness follow you all year through.












With Love,

ATM