Monday, April 25, 2016

Movie: War Room, A must watch

Habari..

Nimekuwa busy na namshukuru Mungu kwa kunipa kuwa busy, wala silalamiki, ila sasa nimewamiss sana.

Sijapata muda wa kuwaletea mada zingine ila leo acha nikupe ushuhuda.
Image result for war room
Mimi nimejifunza kumuamini sana Mungu nikiwa na umri mdogo sana na Mungu hajawahi "kunilet" down hata siku moja. Haimaanishi sipiti magumu....On the contrary, Napita magumu mengi sanaaaa ila Mungu ni mwaminifu kabisa kunivusha.

Na kuna wakati namuuliza Mungu huwa ni kwa nini umeruhusu na hili, guess what na hayo pia anajibu. Kati ya mambo yanayoniweka busy sana sasa hivi ni project from Heaven ambayo Mungu amenipa as an answer to my prayer of WHY THIS LORD?

Najua hapo unaweza usielewe ila hiyo ni mada ya siku ingine na ukiona nimesahau kuileta please nikumbushe kabisa. Email yangu ni tunzo.agape@gmail.com na ukiwa na mada unataka tuizungumze tafadhali drop any comment there

So muujiza wangu mwingine wa very recent ni movie inaitwa War Room, Ok how is it a miracle naona unaweza usielewe ila jamani Mungu wetu ana njia nyingi sana za kujibu maombi yetu na mojawapo kwangu ilikuwa kupitia hii movie. Itafute na namuomba Mungu iwe muujiza kwako pia.

Watch the trailer here
https://www.youtube.com/watch?v=mIl-XY9t_Lw


Happy watching

ATM
Image result for war room
May God answer you when you PRAY

Monday, April 4, 2016

Kumuandaa mtoto wako kwa siku ya kwanza shuleni/Preparing your Child for the first day of school

Hello wasomaji wangu,

So my baby girl ameanza kwenda shule. Jamani yalikuwa maamuzi magumu ila inabidi aende. So ngoja nikupe tips nilizotumia na ambazo watu wengine wametumia sehemu mbalimbali duniani wakiwa wanawapeleka watoto wao shule kwa mara ya kwanza.

Image result for how to prepare your baby for school
1. Chagua shule nzuri.
Hili ni muhimu sana hasa mtoto anapokuwa hana umri mkubwa sana. So mimi nilifanya karesearch kadogo na nilitafuta sehemu ambayo mtoto hatakuwa anafanywa asome sana. Najua hapa wengi mtashangaa ila kwa umri wake sitaki sehemu ambayo atafanywa aweze kuhesabu mpaka 50 kwa miezi miwili....hapana. Nilitaka sehemu ambayo ni playful and fun..sehemu ambayo mtoto anakuwa mtoto. So mfano wa darasa la mtoto wangu wanakaa kwenye vigodoro like a camp, wanalala when tired and anatoka shule saa 6 mchana

2. Mueleze nini ategemee shuleni
Hapa usimwambie "Usiogope yote yatakuwa sawa" "Shule ni raha tu"..hapa ni uongo maana hata sisi wenyewe hatuamini hilo. Mueleze tu atakayoyakuta shuleni, wanafunzi wengi, waalimu kucheza kuimba. Ikiwezekana nenda katembelee darasa atakalosoma na yeye ili aone. Hii ni muhimu sana hasa kama mtoto amefikisha umri na hajawa na hamu ya kwenda shule.

3. Mkutanishe na watoto wengine
Image result for how to prepare your baby for school
Kama mtoto ni wa kwanza na hana majirani anaocheza nao basi ni muhimu kumsaidia kwa kumkutanisha na watoto wengine ili ajifunze social behaviors kama kushare vitu na kuishi na wenzake bila kuumizana. Mkutanishe na watoto wengine na mfundishe Dos and Don'ts.

4. Fikiria njia utakayotumia kuagana naye shuleni
Image result for how to prepare your baby for school
Ukimfikisha mtoto shuleni usimkimbie. Hii inamfanya mtoto aone kama hutarudi. Mueleze kuwa utarudi na hapo muage.
Mnaweza kuwa na goodbye kiss, Hi 5, a short prayer anything that works for you. Mueleze kuwa utarudi kumchukua au kama kuna mtu atamchukua basi mueleze.

5.Msomee mtoto wako
Image result for how to prepare your baby for school.
Hii nimeiandikia sana, kumsomea mtoto kunasaidia sana yeye kuwa na uelewa wa mambo haraka. Kusoma kuhusu umuhimu wa kumsomea mtoto kwako bonyeza HAPA.

6. Msaidie kukuza uwezo wake wa kusikiliza
Shuleni mtoto anategemewa kusikiliza na kufuata maelekezo mbalimbali hivyo ni muhimu mtoto kujifunza kufuata maelekezo mbalimbali.
Hata kama una dada wa kukusaidia kazi nyumbani ni vyema kumtuma mtoto vitu vidogo vidogo hapo nyumbani ili aweze kujua jinsi ya kufuata maelekezo.
Mwambie aondoe vyombo mezani. Mwambie apeleke viatu vyake sehemu ya kuweka viatu n.k.

7. Usilie unapomuacha shuleni hata kama analia
Image result for how to prepare your baby for school
Hii najua ni ngumu kumeza ila muonyeshe mtoto how strong you are na yeye atatulia. Ukilia na yeye atazidi kulia. Jikaze kalie badae. Hahahah...

8. Msaidie kukuza ubunifu wake
Image result for how to prepare your baby for school
Kabla ya mtoto kwenda shule ni muhimu kununua pencils, colors za aina mbalimbali, madftari...muache achore chore tu na kama ni mkubwa msaidie kufanya mazoezi kama kupaka rangi kuunganisha dots, kuunda maumbo na kadhalika. Hii inamsaidia motor skills hasa kujua jinsi ya kushika kalamu.

I wish you a great new beginning.

With love,
Image result for how to prepare your baby for school
Mama GG