Friday, October 23, 2015

Wafundishe kujiamini: Teach them to be confident

Habari za Ijumaa ya leo...

Naamini wiki imekuwa njema sana. Namshukuru Mungu kwa sababu anatutunza. Wiki hii mmoja wa wasomaji wangu wakubwa wa blog hii amepata baby boy. Many congratulation to them Hongera sana Nancy kwa kumpata your champion.


Image result for confident child
Nimekulia kwenye familia yenye baba ambaye ni muhubiri. Baadhi yenu mnaweza msielewe what it means kuzaliwa kwenye familia ya namna hii ila lets say all the complaints I had nikiwa mtoto well, nafurahi kuwa nilizaliwa huko. Anyway, baba yetu anatupenda sana na alikuwa anapenda kwenda na sisi kila anapokwenda, na sie jinsi tulivyokuwa tunapenda safari sasa yaani it was fun UNTIL tulipokuwa wakubwa enough kuweza kufanya utambulisho wenyewe.
Image result for confident child
Tulipofika umri wa kama miaka 13 hivi baba alitaka tujitambulishe wenyewe mbele ya watu badala ya yeye kututambulisha. Ilikuwa inaniogopesha mpaka siku zingine sitaki kwenda naye. Ila nikuambie tu hii imenipa sana confidence ya kusimama mbele ya watu. Haimaanishi kuwa huwa siogopi au sina wasiwasi lahasha imenisaidia kuona ni jambo linalowezekana na inanisaidia kuimprove kila wakati.


Sasa ni kwa jinsi gani unaweza kumsaidia mtoto kuwa confident? Au ni kwa jinsi gani baba yangu aliweza kutusaidia kuwa confident kuongea mbele ya mtu yeyote?

Hizi tips sio za kisayansi ni mbinu alizotumia baba yangu kwa watoto wanne (4) ambao so far tumeweza kwa kiasi fulani kuwa confident, siwezi kusema zinaweza kumsaidia kila mtoto kwasababu watoto wanatofautiana ila kwa ujumla unaweza kuchanganya na mengine na kufuatana na personality ya mtoto.

Tips:
1. Mruhusu mtoto wako kuwa na maoni nyumbani. Familia nyingi za kiafrika baba na mama na zingine baba tu ndo mwenye maamuzi yote nyumbani ila sio hivyo kwetu. Baba alitupa nafasi ya kusema kile tunaona kwenye mioyo yetu bila kutukaripia. Hii ilitufanya kuwa na ujasiri wa kuongea

2. Ruhusu watoto kuongoza mijadala nyumbani. Nimefikiria jinsi ya kuweka hii point. Nyumbani kwetu kila jioni kuna maombi na kila mtoto anasiku yake ya kuongoza in short unakuwa mchungaji wa siku hiyo, hii imetusaidia sio tu kuwa na ujasiri wa kuongoza mjadala ila uwezo wa analyse, kuchambua jambo...hii imetusaidia sana hata katika masomo yetu


3.Waonyeshe watoto kuwa kukosea ni sehemu ya kujifunza. Kwenye kujifunza kokote kuna kukosea kwingi na kama mzazi ni muhimu kuwa mvumilivu na kwa upole kabisa kumuonyesha mtoto njia nzuri ya kufanya jambo. Sikumbuki mimi kuchapwa kwasababu ya kuangusha glass...nakumbuka kuelekezwa cha kufanya nikiwa natumia glass.

Itaendelea...


Yours Truly,
ATM

No comments: