Monday, October 12, 2015

Part 3:Loving your child can prevent them from becoming criminals: Kumpenda mtoto kwaweza kumuepusha kuwa mhalifu

Habari wapenzi wasomaji wangu,

Naamini ninyi na watoto wenu na familia ni wazima kabisa. Natamani nimalizie series hii ya muhimu sana.

Kwenye post yangu ya mwisho nilizungumzia kidogo kuhusu unyanyasaji na leo naomba nielezee halafu tumalizie. Mwaka huu unakaribia kuisha natamani tunapoanza mwaka mwingine tuweke malengo na mikakati mipya kuhusu malezi ya watoto wetu. Hilo nitalizungumzia wiki zijazo.

Tuendelee....


Image result for Child abuseAina za unyanyasaji/Types of child abuse
Kuna aina nne (4) za unyanyasaji wa watoto
  1. Sexual Abuse/ Unyanyasaji wa kingono
  2. Neglect/ Utelekezaji
  3. Emotional Abuse/Unyanyasaji wa kihisia
  4. Physical Abuse/Unyanyasaji wa kimwili
Sexual Abuse:
Any sexual activity, practice or instruction which either meets the criminal definition or is unhealthy for a child considering his/her age and level of development. Criminal activity is defined as “commit[ting] or allow[ing] to be committed any illegal sexual act upon a child including incest, rape, fondling, indecent exposure, prostitution, or allow[ing] a child to be used in any sexually explicit visual material.” - Haya ni matendo yoyote yanayohusiana na ngono, kumshika mtoto maeneo yake ya siri, kumpapasa, kufanya naye tendo la ndoa, kumuonyesha matendo ya ngono, au kuruhusu mtoto afanyiwe matendo haya na mtu mwingine. 

Vitendo hivi hufanyika sana majumbani mwetu bila ya wazazi kujua na mara nyingi watoto wanaogopa kusema. Hivyo ni muhimu kwa wazazi kuwa karibu sana na watoto wao ili wajue vitendo hivi. 

Muuaji mmoja anayeitwa Bobby Joe Long alisema yeye alilazimishwa kulala kitanda kimoja na mama yake mpaka akiwa na umri wa miaka 13 na alilazimika kuona mama yake akifanya mapenzi na wanaume...unaweza kugoogle
Image result for Child abuse
Neglect:
Is defined as failing or refusing to provide adequate food, clothing, shelter, emotional nurturing, or health care. It may also mean failing to provide adequate supervision in relation to the child’s age and level of development - Hii ni pale mzazi anapoacha kumpatia mtoto mahitaji yake ya msingi, chakula, malazi na mavazi, matibabu na ulinzi. Hii wengi wetu tunajitahidi kufanya ila wengine wanashindwa kufanya hasa kwa watoto wa kambo. Hii tunaiona sana kwa watoto wa mitaani na ni jambo la hatari sana hapo baadae kwa taifa

Carlton Gary huyu naye alikuwa muuaji anasema mama yake alikuwa anasahau kumpa chakula na hivyo alilazimika kula kwenye takataka

Emotional Abuse:
 Refers to any acts such as intentional humiliation, causing emotional conflict, or any act that could be psychologically damaging to the child, such as dressing a boy like a girl.Children that are subjected to emotional violence and humiliation by their parents or teachers, lack in self confidence and suffer from emotional problems during adulthood. These individuals caught in the cycle of violence could possibly become violent in adulthood.

Hii wazazi wengi hata wengine wetu tulifanyiwa na waalimu pia, kumtukana mtoto na kumdhalilisha, kumtembeza barabarani akiwa amefanya jambo kama kukojoa kitandani, ni hatari sana. Inaumiza watoto na kwa sababu hawezi kusema anaishia kuwa na kutojiamini na kuishia kuwa na maumivu na hasira inayoweza pelekea kuwa mhalifu
Image result for Child abuse
Physical Abuse:
 Is defined as causing or allowing any non accidental physical injury. 

Hii naomba nieleze kwa upole kabisa, wengi tumechapwa ila kuna wazazi wanaoumiza watoto kabisa eti wanawafundisha adabu. Ni muhimu kufahamu kuwa kumuadhibu mtoto kuna mipaka na sio kumuumiza. Ni muhimu kutokutoa adhabu ya kumchapa mtoto unapokuwa na hasira kali au unapokuwa na msongo wa mawazo. Ni muhimu kutulia na kutoa adhabu kwa umakini mkubwa sana.

Mbakaji na muuaji mmoja anaitwa Lorenzo Fayne yeye alikuwa anapigwa kichwani na mama yake.

Tafadhali share na sisi jambo lingine linalohusiana na unyanyasaji wa watoto.

Tafadhali wajulishe wengine kuhusu blog hii tuponye kizazi chetu.

Image result for Child abuse
ATM

No comments: