Tuesday, September 29, 2015

Part 2:Loving your child can prevent them from becoming criminals: Kumpenda mtoto kwaweza kumuepusha kuwa mhalifu

Habari mpendwa mzazi,

Kwenye post yangu ya mwisho nilianza hii mada ya kumpenda mtoto, na leo naomba nielezee kuhusu Child Abuse, au unyanyasaji wa watoto ambao umeonekana kuwa chanzo kikubwa sana cha kusababisha watoto kuja kuwa wahalifu wanapokuwa watu wazima.

Image result for it shouldnt hurt to be a child
Ni muhimu kufahamu kuhusu unyanyasaji huu maana inawezekana ukawa unaufanya au ulishafanya bila kujua au kuna mtu karibu anafanya na hujajua kuwa ni unyanyasaji na hivyo kufahamu kunaweza kusaidia jamii yetu kuacha huu unyanyasaji. Ni muhimu pia kujua kwa sababu jamii ya kitanzania tunakuwa na familia kubwa sana, mzazi kufahamu kuhusu huu unyanyasaji unaweza kufundisha watoto wako na hivyo ikawasaidia kujikinga na matukio kama hayo kama yatatokea kwao ukiwa haupo nao.

Kwenye post ya nyuma tumeona kuwa familia ni sehemu ya muhimu sana ya ukuaji wa mtoto, ni hapa ambapo identity ya mtu inatengenezwa, na kama mazingira ya nyumbani hayako vizuri kwa ukuaji wa mtoto itamuathiri mtoto kisaikolojia. Ni muhimu pia kukumbuka kuwa sio kila mtoto anayekuwa kwenye mazingira mabaya anakuja kuwa mbaya ila inachangia kwa asilimia kubwa sana.

Image result for child abuse
Mazingira mabovu au hatarishi haimaanishi kuishi kwenye nyumba ambayo si ya kisasa, hasha, mtoto anaweza kuishi kwenye gorofa na nyumba nzuri sana yenye kila kitu ila akawa kwenye mazingira hatarishi.

"There is no doubt that direct experience with violence and neglect during childhood, increases the risk of violent behavior during adulthood. However not all children victims turn to violence later in life."

Unyanyasaji wa mtoto ni nini? What is Child Abuse?

Shirika la afya duniani (WHO), wemeeleza unyanyasaji wa watoto kuwa ni, "is any behavior directed toward a child by a parent, guardian, care giver, other family member, or other adult, that endangers or impairs a child’s physical or emotional health and development."-ni tabia yoyote inayoelekezwa kwa mtoto na mzazi , mlezi, mtoa huduma , mwanafamilia, au watu wazima wengine , ambalo linahatarisha au kuzuia maendeleo ya kiafya ya mtoto kimwili au kihisia.

Aina za unyanyasaji/Types of child abuse
Image result for it shouldnt hurt to be a child
Kuna aina nne (4) za unyanyasaji wa watoto
  1. Sexual Abuse/ Unyanyasaji wa kingono
  2. Neglect/ Utelekezaji
  3. Emotional Abuse/Unyanyasaji wa kihisia
  4. Physical Abuse/Unyanyasaji wa kimwili

Itaendelea............

ATM


No comments: