Wednesday, September 16, 2015

Part 1: Loving your Child can prevent them from becoming criminals: Kumpenda mtoto kwaweza kumuepusha kuja kuwa muhalifu

Habari wapenzi wasomaji,

 "There is no doubt that direct experience with violence and neglect during childhood, increases the risk of violent behaviour during adulthood. However not all children victims turn to violence later in life. " Maryam Falahati.

Image result for violence in children's drawings
Wiki iliyopita nilikuta kwenye page ya Youtube kwenye laptop yangu, makala inayoitwa "Deadly Women", nilidhani ni tamthilia baada ya kuitazama nikagundua ni habari za ukweli za wanawake katili sana duniani wauwaji. Kusema ukweli inasikitisha sana. Nilisikitika kuona kuwa mwanamke anaweza kuwa katili kiasi cha kuua mtu na kupika nyama yake....jamani ni hatari sana.



Image result for loving my child
Sasa lililonisikitisha sana na kusababisha nitengeneze post ya leo ni ukweli kuwa story za hawa wanawake makatili hivi, zinaonyesha kuwa maisha yao ya utotoni hayakuwa mazuri kabisa. Na wengine mazingira ya familia zao majumbani yaliwapelekea kuwa hivyo walivyo. Sasa mie nikaona nije kushare na ninyi kautafiti kadogo sana nilichokifanya baada ya kuangalia hiyo makala, maana kama tunataka kupona tuambiane haya mapemaa.

Katika Jarida la polisi la saikolojia ya makosa ya jinai la mwaka 2005 walichapisha haya,

 "Perhaps one of the most interesting factors contributing to the development of a serial killer is abuse that is experienced in the killer’s childhood. Childhood abuse has been given varying levels of blame in the development of serial killers. De Becker (1997) quoted Ressler’s research and stated that “100 percent [of serial killers] had been abused as children, either with violence, neglect, or humiliation” (p. 55). Ressler and Shachtman (1992) report that, “over 40 percent of the [serial] murderers reported being physically beaten and abused in their childhoods. More than 70 percent said they had witnessed or been part of sexually stressful events when young…” (p. 85)." Journal of Police and Criminal Psychology, 2005, Volume 20, Number 1.


Image result for loving my child
Yaani ni hivi hao watu wanaoitwa serial killers, yaani mtu anayeua watu zaidi ya watatu katika matukio zaidi ya matatu tofauti, asilimia 100 ya hao watu walifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wakiwa watoto. Zaidi ya 40% ya hao wauwaji walipigwa na kudhalilishwa wakiwa watoto na zaidi ya 70% wamekuwa mashahidi au wamekuwa sehemu ya vitendo vya kingono wakiwa watoto. Hii ni hatari.



 "The family is the most important and the original institution of society for bringing up and protecting children. However this same institution can be the cause of violence, pain and suffering. All over this planet, women and children are murdered, maimed, are assaulted and battered, and sold. Millions of human beings are suffering in the confines of their families, and unfortunately knowledge and information about this is only the tip of the iceberg, an iceberg that still many believe it to be their private domain." Maryam Falahati.

Itaendelea......

ATM

No comments: