Thursday, September 3, 2015

Books! Books! Books! Vitabu! Vitabu! Vitabu!

Habari za siku nyingi?

Sijaposti siku nyingi ila mambo yote ni mema.

Nilipokuwa na mimba ya miezi kama mitano( 5)/sita (6) hivi nilipita kwenye bookshop moja na kununua vitabu vitatu (3) kwa ajili ya Genesis. Hivyo ndio vilikuwa vitu vya kwanza kabisa nilivyonunua kwa ajili ya mtoto wangu.

Wazungu wanasema, "A child can not have too many books" (Mtoto hawezi kuwa na vitabu vingi kupita kiasi).

Najua wengi wetu hatuna mazoea ya kusoma vitabu na sijui kama wengine mnatamani kama mimi kuwa kizazi chetu kiwe tofauti.

Nilipokuwa O'level nilipata bahati ya kusoma na watu waliokuwa very talented (Nitaleta habari zao hapa siku nyingine), hawa watu walikuwa wakifanya vizuri sana darasani na nilijua siri yao ilikuwa ni nini, WALIKUWA WANASOMA SANA VITABU. Ngoja nikwambie hakuna short cut ya kulisha akili yako na ya mtoto wako zaidi ya kusoma vitabu SANA.

Baba yangu alitusomea sana vitabu na jamani amejitahidi kununua vitabu sana kwa ajili yetu, baadhi ya vitu ninavyojua leo nisingejua kama isingekuwa juhudi ya baba yangiu ya kutusomea vitabu jioni.

Baba yangu hana elimu kubwa sana ila anajua mambo meengi sana kuna wakati nilidhani ananidanganya maana kila swali nikimuuliza anajibu lake, ila nilipokuwa mtu mzima kidogo niligundua kuwa baba yangu anapenda kusoma sana jamani, anasoma literally kila kitu.

Wataalamu wa mambo ya watoto wanasema ni vema kuanza kumsomea mtoto akiwa tumboni...soma tu maana anauwezo wa kusikia sauti yako na anapozaliwa anza kumsomea, haelewi maneno yako ila anajifunza kuwa msikivu (jambo ambalo ni adimu sana).

Kuna faida nyingi za kuanza kumsomea mtoto wako mapema, chache ni


  • Inasaidia kuongeza na kujifunza misamiati
  • Inachochea uwezo wa mtoto kujenga picha ya jambo (Imagination)
  • Inafundisha ujuzi wa kuwasiliana (Communication skills)

Kama umewahi kusoma kitabu kinachoitwa Gifted Hand kilichoandikwa na Ben Carson unaweza kuelewa ni nini maana ya kupenda kusoma vitabu, tabia ya kusoma vitabu ilimsaidia Dr. Ben kutoka kuwa wa mwisho darasani mpaka kuwa daktari bingwa wa matibabu ya kichwa duniani. Kwanini wa kwako asisome?

Kama unataka kumnunulia mtoto zawadi, kanunue vitabu, hutajuta

Make a difference, read books, be the difference, be their role model.

Bonyeza link hapo chini kwa taarifa zaidi:



ATM.

No comments: