Tuesday, March 24, 2015

Part 3: Healthy living: Mabadiliko wa mfumo wa maisha

Hello my lovely readers.....

I have been very busy but I am healthy and I thank God. Hii ni part ya mwisho ya maamuzi ya kubadili lifestyle.

Leo ningependa kuzungumzia hatua za kufuata ili uweze kuishi maisha yenye afya bora.

Si mtu mnene tu anayepaswa kuishi maisha yenye afya, ni wajibu wa kila mmoja. Kuna watu wembamba wanaokula chips na junky food siku nzima, ingawa hujanenepa afya yako si bora. Ukifuata kanuni za ulaji bora wa chakula hata mwili wenyewe utaanza kupungua kama umnene.

Hatua za kufuata:

1. Acha kula vyakula vyenye mafuta mengi. Mafuta ni mazuri kwa afya ila mafuta mengi na mafuta yaliyokuwa refined sana si mazuri kabisa. Hii inamaanisha punguza kukaanga vyakula, badala yake choma, chemsha au pika kwa mvuke.

2. Punguza au acha kabisa kula "processed food" hii sijui kiswahili chake ila vyakula vya viwandani na vya makopo si vizuri sana maana havina virutubisha vyote na vimeongezwa kemikali ambazo si nzuri. Pika vyakula mwenyewe na kula vyakula ambavyo havijakobolewa.

3. Ongeza ukijani na rangi mabali mbali katika mlo. Wanasema kizungu, "Make your meal more colorful". Kula mboga mboga na proteins na punguza wanga. Ongeza pia mlo wa matunda. Matunda yana sukari asili na hivyo ni nzuri kwa afya kuliko sukari ya kiwandani.

4. Fanya mazoezi. Mazoezi yapo ya aina nyingi, wanasema ukitembea lisaa 1 kwa wiki ni nzuri kuchangamsha mwili. Fanya kazi za nyumbani cheza na mtoto, fanya kitu...usikae tu.

5. Kunywa maji. Wote tunajua umuhimu wa maji mwilini. Kunywa maji yasipungue lita 2 kwa siku. Hii itasaidia kuondoa hamu ya vinywaji visivyo na afya kama soda, bia na juice za viwandani.

6. La mwisho pata muda wa kutosha wa kupumzika. Lala kwa angalau masaa 8. Usingizi ni muhimu sana, hakikisha unapumzika na mchana uwe na muda wa kurelax ukisoma kitabu au kutulia tu.

Ukifuata kanuni hizi chache itakuwa mwanzo wa maisha ya afya bora na kupunguza uzito na magonjwa yasiyo na lazima.

Anza leo.

ATM

No comments: