Thursday, February 19, 2015

Mbinu za kupunguza kutema mate sana ukiwa mjamzito

Habari wapendwa,

Nisameheni nimekuwa kimya kuna jambo limenikeep busy sana siku moja nitashare hilo jambo. Jamani napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa support ya kutembelea hii blog na maoni mnayotoa. Yananitia sana moyo na ninafarijika kuwa nina watu wanaosaidika.

Post ya leo imetoka kwa moja ya my reader, labda my number one reader, Nancy, asante sana Nancy, nakupenda sana.

Kwa wale ambao mlishawahi kuwa wajawazito na mlio wajawazito sasa mnajua dhiki ya kutema mate sana. Sasa leo naomba niwaambie vile vitu vinaweza kuwasaidia ambavyo vimesaidia wanawake wengine.

  • Kata vipande vya limao/ndimu vidogo vidogo weka kwenye mfuko wa nylon, unaweza kutembea navyo kwenye pochi, ukijisikia unataka kutema mate nyonya kipande kimoja na hali itaisha
  • Jaribu kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya vitu vyenye sukari na sukari yenyewe. Sukari inatabia ya kuongeza uzalishwaji wa mate kwa hiyo ukipunguza kula sukari uzalishwaji wa mate utapungua
  • Weka unga wa kahawa chini ya ulimi, hii inasaidia kunyonya unyevunyevu unaosababishwa na mate, hii itakufanya uone kama unakunywa kahawa 
  • Kwa wale wanaokaa maeneo yanayolima alizeti, ukinyonya mbegu za ua la alizeti inaondoa hali ya kutaka kutema mate na hii inaonekana kusaidia wanawake wengi sana

Tafadhali mjulishe mtu mwenye hali hii na utakuwa msaada mkubwa.

Again many thanks to Nancy for an amazing information. Love love love

See you.

ATM

No comments: