Wednesday, February 25, 2015

Chunusi wakati wa ujauzito; Kwanini na nifanyeje?

Habari wapendwa wasomaji wangu,

Kwanza napenda kuwashukuru sana kwasababu ndani ya kipindi kifupi nimekaribia kufikia views 1000. Ni hatua nzuri na inatia sana moyo.

Nashukuru Nancy kwa kupendekeza topic hii. Big up Nancy.

Wataalamu wanasema ingawa haijajulikana haswa kwanini wanawake wanapata sana chunusi/pimples wakati wa ujauzito ila inaaminika chunusi husababishwa na ongezeko la homoni hasa miezi mitatu (3) ya kwanza ya ujauzito na kufanya mafuta ya kwenye ngozi kuongezeka na hivyo kusababisha chunusi. Ni jambo la kufurahi pia maana inaonyesha kuwa uko vizuri.

Tahadhari
Chunusi huwa hazifurahishi, ila wataalamu wanashauri,

  • Usibinye wala kukwangua chunusi kwasabu zitaacha madoa kwenye ngozi
  • Usitumie dawa za kununua dukani maana dawa hizi zinaingia kwenye mishipa ya damu na hivyo yaweza kumdhuru mtoto.


Nifanyeje?

  • Osha uso mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni, na usisugue uso kwa nguvu wakati wa kuosha
  • Badili vyakula unavyokula, kula vyakula ambavyo ni antioxidants kama mboga mboga, matunda hasa yale yenye uchachu, samaki, na epuka kutumia mafuta mengi kwenye chakula na kama unaweza tumia Virgin Olive oil kupikia. Mfumo huu utamsaidia hata mtoto wako tumboni
  • Usitumie sabauni zenye mafuta na kemikali kali na kama una ngozi yenye mafuta osha nywele kila siku
  • Kama unapaka sana make-ups hakikisha kuwa hazina mafuta
Habari njema ni kuwa baada ya muda chunusi huisha na utarudi kuwa na ngozi yako ya kawaida kwa hiyo vumilia tu.

Nawapenda.

Agape

No comments: