Thursday, May 14, 2015

Love, Pain and Death: A true sad story. part 2

Habari,

Naamini wote ni wazima. Sehemu ya pili na ya mwisho ya simulizi hii. Tafadhali jifunze na chukua hatua inapostahili.


Image result for sad story about love
"Mtoto wa pili alipofika miaka mitatu, alipata kazi, akaanza kufanya kazi na kupendeza kidogo...siku hiyo from no where mumewe akaenda kazini kwake akafanya fujo na kuwaonya wasimuajiri mkewe, akafukuzwa kazi.......

Lakini hakusema, tukawa hatujui....baadae manyanyaso yakawa makali ikabidi arudi nyumbani na wanawe, sasa baba mkubwa alipomuuliza alimwambia tu kua ndoa ngumu bila kufafanua, basi akaamriwa arudi kwa mumewe; 

Alikuaga mkimya sana, akarudi kwake.....kumbe miaka yote toka aolewe mumewe alikua na mazoea ya kumpiga bila huruma!

2014, Alibeba mimba tena na January mwaka huu alipata mtoto wa kiume(ameachwa na 4month mwezi wa tano haujaisha)  akiwa kajifungua mumewe hakumjali hata chembe, alimnyima hata pesa ya chakula.....mtoto akiwa na wiki mbili aliomba chakula kwa mumewe akapigwa kama kawaida......kumbe aliumia sana damu ikavia kwenye ubongo......akaparalyz 

Kuna msamaria alimwambia shangazi etu kua mwanenu anaumwa hoi na kafungiwa ndani.....ndio kwenda na kumkuta yu taabani kwa njaa na paralysis......na kichanga chake...

Akarudishwa nyumbani na kupelekwa muhimbili....baada ya kupata nafuu na kuweza kuongea ndio akahadithia mateso alokua akipewa na mumewe....baba mkubwa alilia sana na kumlaumu kwanini hakua muwazi toka mwanzo.....basi akiwa anauguzwa mumewe akiambiwa juu ya matibabu ya mkewe anasema hana hela......wakamuacha tu!

Alipopata nafuu akaomba kurudi rombo apumzike hadi afya irudi na ilikua zifanyike taratibu za kikanisa kuwatenganisha......bahati mbaya kumbe aliumia ndani ya tumbo pia.....so alipokuja rombo aliumwa tena tumbo na kuonekana kuna damu inavuja tumboni......akafariki "


Nawatakia siku njema.

No comments: