Monday, May 11, 2015

Love, Pain and Death: A true sad story. Part 1

Habari wasomaji wangu,

Naamini wiki imekuwa njema na kina mama mlisherehekea siku yenu kwa furaha.

Nimepata hii hadithi mahali, nimeona nikushirikishe. Ni habari ya kweli kabisa na ni ya hapa hapa Tanzania.

Natamani ujifunze jambo hapa na umsaidie mwanamke mwingine anayepitia kipindi kama cha dada huyu.



"Huyo dadaangu aliolewa2009 akiwa mjamzito na mapema 2010 alipata mtoto wa kike. Mumewe hakufurahia kwasababu mke alizaa mtoto wa kike na hafanani na baba. Bahati nzuri alitoka uzazi na mimba nyingine, na 2011 alipata mtoto mwingine wa kike na hafanani na baba yaani watoto hawa ni copy ya mama yao. 

Jinsi mumewe alivyotaniwa na majirani kua watoto hawafanani nae alipata hasira zaidi sababu alitaka mtoto wa kiume sana.....basi kulingana na hali hiyo dadaangu aliachishwa kazi na baada ya mwezi mume akafukuza house girl kwahiyo dada akabaki mwenyewe na hivyo akawa anapata tabu ya majukumu nyumbani na watoto wake wadogo.

Ndugu wa upande wetu tukawa tunamsaidia maana mume alikua akiacha 2000, sasa DSM 2000 na watoto unaifanya nini? Mumewe kuona tunampa msaada akaamua kutafuta nyumba mbali huko Mbagala ndani, akamnyang'anya simu na akapiga stop ndugu wa mke kufika kwake na ilifikia hatua akamtukana shangazi yetu kua ni mchawi wa ndoa yake.

Tulimtafuta tukajua anapoishi, ila dada alikua tayari kuvumilia ndoa yake akijua watoto wakikua atatafuta kazi na kujimudu."

Image result for sad story about love

..........itaendelea.

Nakutakia wiki yenye baraka tele.

ATM


No comments: