Friday, March 6, 2015

Healthy Living: Mabadiliko ya mfumo wa maisha.

Habari.....

Kuna wakati nilikuwa kimya kidogo na niliahidi kuwa nitasema kwanini.

 Kwa muda sasa nimekuwa nikisoma blogs na kufuatilia watu kadhaa katika mitandao na jambo ambalo ni trending now ni Healthy Living.

Kwa ufupi ni kuwa watu wameamua kuishi maisha yaliyobadilika na kuwa ya afya njema zaidi. Watu wameamua kubadili mfumo wa maisha kabisa na wanaishi kwa furaha zaidi.

January mwaka huu nilihamia Mwanza na baada ya muda mfupi nilianza kuexperience maumivu ya goti yasiyo ya kawaida. Nilikuwa nashindwa kuchuchumaa, kwa kweli nilikosa raha. Niliamua kupima uzito maana nilihisi hiyo shida ni kutokana na uzito mkubwa. Baada ya kupata majibu ya uzito yalinishtuka sana na niliamua kucheck BMI, Body Mass Index, kipimo hiki kinapima ratio ya urefu na uzito na majibu yalikuwa kuwa mimi ni OBESE, yaani ni mzito kupindukia na niko katika hatari ya kupata magonjwa
kama ya sukari, presha na moyo. Siku hiyo nilirudi nyumbani nikamwambia mdogo wangu kuwa sitakula chakula tena.

Siku iliyofuata nilianza kutafuta diet mitandaoni na niliwaambia watu ofisini kuwa nataka kuloose weight. Waliniambia sitaweza na nisihangaike. Nilifanya maamuzi magumu na nikaanza diet mwezi mmoja na wiki moja iliyopita.

Mpaka sasa nimeshapunguza kilo 7 na mapambano yanaendelea. Wengine wanaweza kuona kuwa kilo hizi ni kidogo sana kwa kipindi hichi ila kwa kweli I am so proud of me.

Post ijayo nitaendelea na mada hii.

Badili maisha yako leo.

ATM

No comments: