Tuesday, January 27, 2015

Je, nitazaa mtoto mlemavu au?

Sijui ni wangapi wenu mmeshawahi kujiuliza swali hili wakati wowote...inawezekana bado hujawa mjamzito ila umeshawahi kujiuliza na hasa kama katika familia kuna watu wenye ulemavu tofauti tofauti....inaogopesha sana.

Kabla sijafahamu kuwa ni mjamzito niliumwa kwa kama miezi miwil hivi na nilikunywa antibiotics kali sana. Zote zilikuwa zimeandikwa " Not to be used by women in their first trimester", yaani hazikupasa kutumiwa na wanawake wajawazito walioko kwenye miezi 3 ya kwanza.


Hapo ndo nilipoanza mawazo sana kuwa mtoto atakuwa kiziwi au kipofu au vipi. Daktari aliniambia nitajua matokeo nitakapojifungua. Iliniogopesha, niligundua kuwa siwezi kumwambia Mungu usinipe mtoto mlemavu...apewe nani sasa?

Niliyofanya:

  • Nilimwambia Mungu mapenzi yake yatimizwe
  • Nilimwomba Mungu anipe nguvu na upendo wa kulea mtoto hata kama atakuwa mlemavu
Baada ya maombi hayo mafupi nilikuwa "stress free" and was waiting anxiously for my surprise from God

Happy parenting,

No comments: