Thursday, April 23, 2015

Lini nianze kumpa mtoto chakula kipya?

Habari za leo,

Nimefurahi sana nimepata feedback nyingi sana kutoka kwenu na inanipa hamasa ya kufanya zaidi.

Mada ya leo ni nyeti sana na nitakachokueleza hapa ni kile nilikipata kwenye mtandao wa babycenter.com. ilinipa mimi mwongozo naamini hata wewe itakusaidia.

Image result for when should i introduce other meals to an infant
Nilipopata mtoto sikuwa na kazi na hivyo nilikuwa na muda wa kutosha kukaa nyumbani na kutunza mtoto na hivyo niliamua kuwa nitamnyonyesha mtoto exclusively (maziwa ya mama tu) kwa miezi 6. Hii inamaana mtoto alinyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi chote hiki.

Baada ya hapo nilianza kumpa:

  • Uji mwembamba wa dona wenye maziwa ya kutosha, uji niliuchuja na nikawa nampa vijiko vitatu (3) mpaka vitano (5) tu. 
  • Nilimpa pia viazi vilivyopondwa pondwa na maziwa
  • Nilimpa pia maboga na butter nut yaliyopondwa na maziwa 
  • Nilimpa pia ndizi, maparachichi, apples zilizopondwa poandwa
Unaweza pia kumpa cereals ukichanganya na maziwa ya kutosha, ila iwe ya aina moja.

Tips:
  • Ukimpa mtoto kitu kipya subiri kwa siku kama 3 hivi kabla hujampa chakula kingine ilikuona kama mtoto ana allegy na chakula husika.
  • Mpe chakula kipya muda mfupi baada ya kunyonya kama baada ya lisaa limoja, asiwe na njaa sana
  • Kama unampa uji au cereals ongeza uzito kadiri siku zinavyoendelea
  • Mpe mtoto chakula mara moja kwa siku kama ana umri chini ya miezi 6 na mara 2 kati ya miezi 6-7  na ongeza kadiri muda unavyoendelea.
  • Tumia kijiko cha plastic kumlisha mtoto ili usiumize fizi
  • Ukiona mtoto anaacha kufungua mdomo au anageuza shingo pembeni au kuchezea kijiko acha kumlazimisha uwezekano ni kuwa ameshiba au chakula hajakipendaImage result for when should i introduce other meals to an infant
  • Kama mtoto hana allegy na chakula rudia mara kadhaa kabla hujasema mtoto hapendi chakula fulani, mpe muda kukizoea, na atakula kingi zaidi
  • Kama unampa mtoto chakula ambacho kiko tayari kwenye kopo usimlishe moja kwa moja kutoka kwenye kopo, mimina pembeni ili kisipate bacteria.
  • Image result for when should i introduce other meals to an infant
  • Usishangae pale kinyesi cha mtoto kitakapobadilika rangi na harufu, hii inatokana na chakula kipya anachokula
  • Unapompa mtoto chakula usijaze kijiko mpe kidogo tu pale mwanzo wa kijikoImage result for when should i introduce other meals to an infant
  • Hakikisha chakula kinakuwa sio kigumu, weka maziwa ukifanye kilaini kwa wastani
  • Image result for when should i introduce other meals to an infant
  • Mpe mtoto maji kidogo kama milita 60 ili asipate shida ya choo, na kama chakula unachompa kinampa shida ya choo kibadili
  • Mtoto chini ya umri wa chini ya mwaka 1 usimpe ASALI

Image result for when should i introduce other meals to an infant

Have a happy day.

ATM

No comments: