Friday, January 30, 2015

Je niangalie jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa?

Helloo,
Jana mtu aliniuliza kama niliangalia jinsia ya mtoto wangu kabla hajazaliwa. Hii ni kati ya "Dillema" ambayo wengi wanakuwa nayo mtoto akiwa tumboni hasa mmoja wa wazazi anapotaka sana kujua.
Turudi kwangu; of course nilitamani sana kujua jinsia kwasababu nilitamani niandae nguo za mtoto na kuamua jina,siku kadhaa kabla ya ultra sound ambayo ilikuwa niende kuangalia nilipoenda clinic daktari aliniuliza kama najua jinsia nikamwambia ndio nimepanga kwenda kuangalia.

Daktari aliniambia naomba nikushauri usiende, nikamuuliza kwanini? Liniambia,

  • Kila mtu ana hamu ya aina fulani ya mtoto hata kama ungepata yoyote ungefurahi ila kule ndani ya moyo sana kuna unachotamani zaidi
  • Alisema kuna uwezekano wa kuwepo a small disappointment kama jinsia ya mtoto itakuwa sio ile unayoitamani sana. Alisema hii disappointment kwa mama inaondoa furaha ya kubeba mimba na kama atajifungua kawaida (natural birth) morale ya "kupush" inapungua.
  • Lastly alisema it is fun to wait for the surprise...alisema the excitement ya kujua jinsia ya mtoto akiwa amezaliwa it is fulfilling.
Kwa hiyo mimi sikuangalia tena and YES the waiting was worth it. 

Hayo yalikuwa ni mawazo ya daktari na maamuzi yangu. Nilipofanya maamuzi ya manunuzi ya nguo nilinunua nguo zenye 'neutral colors'. Halafu nilikuwa na issue ya rangi za blue na pink ambayo nitashare na nyie siku nyingine. Kuhusu majina nilichagua majina mawili la kike na la kiume
Mwisho wa siku unahaki ya kujua na kutojua. Do what you feel best.

Weekend njema,
ATM.

No comments: