Showing posts with label They Inspire me. Show all posts
Showing posts with label They Inspire me. Show all posts

Wednesday, December 14, 2016

Fashion Alert: How to dress your baby bump (Jinsi ya kuvaa wakati ukiwa mjamzito)

Welcome back,

Ni siku nyingi tangu nimepost jamani. Namshukuru Mungu mimi ni mzima na ninyi pia. Well tuko kwenye the best season of the year and well what a better time to talk fashion than now eeeh. Okey. So hii post nilitaka niiweke siku nyingi sana ila nikawa nimebarikiwa na kazi nyiingi ila naamini sijachelewa.

Hapa Tanzania watu wengi tunakuwa na tabia ya kuvaa vaa tu tukiwa wajawazito, mitandio inaongezeka, sijui kwanini tunapenda kuficha hizo baraka. Na wakati mwingine tunajichukia sana tukiwa wajawazito na ni kwasababu hatujui kuvaa mavazi ya kutupendeza na yenye heshima.

Naomba nitoe angalizo kwa posti hii. Kama haujisikii kubanwa basi nenda na option ambayo ni loose. Na kama kiatu kirefu hukiwezi basi we vaa tu flat. Ni muhimu kuinvest kwenye materinity dress nzuri maana wengi bado zoezi linaendelea na zinaweza kuwa handy. Ila pia nitapost jinsi unaweza kufanya matenity dress yako ikavaliwa vizuri tu baada ya kujifungua.

Basi for inspiration ya leo, nimemchagua mwanadada Anitha. Ni fashionista hapa Tanzania na akiwa mjamzito well, she doesn't disappoint. Asante Anitha kwa kuniruhusu kutumia picha zako. Be blessed and keep slaying

Unaweza kumfollow Anitha instagram kama anithascloset au utembelee blog yake. Click here kwenda kwenye blog yake.



To be continued......
Cooperate look



Working on a couple of posts for the blog on this fine thursday morning...thank you Mr.president for a public holiday... perfect weather for it...God bless Tanzania! 
#greenforgreen #anotherbumpshot #mothersinprotest #tbt




Thursday, May 26, 2016

Agape's 5km Marathon

Habari za siku nyingi,

Naamini muwazima na mmeshapata nakala zenu za video ya War Room.

Image result for life is like a marathon
Wiki iliyopita nilipata bahati ya kushiriki marathon moja hivi na nikakimbia kilometa 5. Nilipoenda kama mita 200 nilikuwa nimechoka sikuwa na viatu sahihi vya kukimbilia,niliamua nitatembea badala ya kukimbia tu. Baba mmoja ambaye naye alishiriki alikuwa amechoka ila aliniambia mama twende. Kila akitangulia mbele yangu kidogo aliniambia jitahidi, twende etc. Na kila akisema hivi naongeza mbio au mwendo alifanya hivi mpaka nilipomaliza
Image result for life is like a marathon

Mbio zilifanyika barabarani kwa hiyo palikuwa na watu wanaoangalia. Kuna walioamua kunicheka tu bila sababu,wengine waliniambia kimbia dada unaweza tu. Wengine waliniambia siwezi chochote niache tu. Wengine walinitukana. Wengine waliniambie nipande baiskeli zao na pikipiki mpaka daladala. Wakati nakaribia kumaliza mbio mtu mmoja aliniambia wewe kwanza hata hujakimbia, ulikuwa umekaa tu mahali umejificha ndo umetoka ili umalize. Wewe huwezi kitu.

Wakati wa mbio mara nyingi nilitamani kuacha ila huyu baba ambaye na yeye alikuwa kwenye mbio hakuruhusu aliendelea tu kuniambia twende, fanya bidii. Usiache. Wakati wa mbio niligundua kuwa huyu baba hakuangalia nyuma kabisa, he kept going and looking forward, he was tired but he went and looked forward. Aliniambia, "Nawaangalia wale walioko mbele yetu, karibu tunawafikia". I doubted maneno yake ila we kept going.


Image result for life is like a marathon
Hii ilinifundisha somo kubwa sana kuhusu maisha. Life is like this marathon. Unafanya jambo ila kuna mambo mengi yapo njiani. Utakutana na watu wa aina nyingi kama hawa ambao nilikutana nao mimi. Wengine watakupa moyo, wengine watakukatisha tamaa wengine watakucheka, wengine watakutukana na kukudhihaki.

Cha muhimu kabisa ni PUT ON THE RIGHT SHOES, songa mbele. Never look back, look those who are before you. You went through a bad life experience, never look back look forward. In life keep moving, it does not matter how you move. Run, walk,crawl, just move. Mambo yanaweza kuwa magumu hakuna kukata tamaa, hairuhusiwi kukata tamaa, hakikisha unamaliza what you started.

Hata kwenye malezi ni hivyo hivyo. Kumbuka wewe ni mama au baba bora. Tia bidii. Omba, fanya kila kinachowezekana kufanyika kulea watoto vizuri. Hakuna mzazi perfect duniani. Tunakosea ila tunasahihisha tunasonga mbele tu.

Run your marathon well.
Image result for life is like a marathon

With love,
ATM

Monday, August 3, 2015

For the love of fashion: Meet Zoe Glorious

Habari,

Naamini wewe ni mzima. Samahani kwa kuwa kimya sana, ila mambo yote ni mema. 

Kwa kipindi cha kama miezi miwili nitaweka posts za watu ambao ni ordinary na wanafanya mambo mazuri na wana-inspire wengi. 

Leo naanza na Zoe Prudence Shoo


Image result for zoe malaika glorious
Nimemfahamu Zoe nikiwa Shinyanga Commercial Institute. Siku ya kwanza nimefika shule (Tulikutana bafuni....hahahaha).  Ndani ya dakika chache urafiki ulizaliwa.

Nilisema mimi napenda fashion ila Zoe ni fashion Icon, yaani akiwa mbele ya kioo is all fashion. Watu waliosoma Shycom wanaweza kukueleza jinsi Zoe alikuwa anapenda sana kupiga picha and she had her heart in all the pictures she took. Sisi tuliona ni ordinary pictures ila kwake it was a way of making her identity. 

A fashion Icon.

Nilipomuuliza Zoe aniambie kuhusu yeye kwa kifupi aliniambia yeye ni Creative, Zoe has the ability to think outside the box na kukupa jambo la tofauti, haogopi kuthubutu na hilo ni jambo ambalo linamfanya yeye kuwa mtu wa tofauti sana na kati ya watu ambao ningependa kufanya naye kazi huko baadae ni yeye.

Nilipokuwa nawaza kuhusu Creativity ya Zoe niliwaza kuwa ili Zoe aweze kuwa mtu creative ilihitaji kuwa na wazazi waelewa. Nimepata bahati ya kukutana na mama yake na nilijua kwanini Zoe ni mtu wa tofauti sana.
Image result for zoe malaika glorious 
Wazazi tuna nafasi ya muhimu sana ya jinsi watoto wetu wanavyoweza kuja kuwa wanapokuwa watu wazima. Naamini kwenye kumruhusu mtoto kuwa na imagination na kumtia moyo na sio kumkataza kila  jambo, tunawawekea vikwazo katika kubuni mambo kwenye maisha. Mtoto wangu ana potty ambayo inakuwa assembled upya kila anapoitumia…alipoanza kutumia tulimpa nafasi ya kurudisha potty katika hali yake ya mwanzo na ni jambo analo weza sana.

Jambo lingine ni kumruhusu kutumia vyombo vyote, hata vinavyopasuka. Genesis hajafikisha miaka miwili ila anajua kuwa chombo hiki ni delicate na kina hitaji extra care na kwa jinsi hiyo anakuwa na confidence. Haya ni mambo madogo ila yanaweza kuleta impact kubwa kwa mtoto

Zoe ni mtu ambaye ana huruma na upendo wa ajabu, ni kati ya watu jasiri sana niliowahi kukutana nao. Ni mtu mwenye sincere heart na nimekwambia hapo juu kuwa nilipokutana na mama yake nilijua kwanini. Jinsi tunavyowapenda watoto wetu na kuwalinda inawapa confidence katika jamii ila pia inawasaidia kuwapa watu wengine the same amount of love they have received from us. Wapende watoto wako sana it can change the world.
Image result for zoe malaika glorious
Jambo la muhimu sana la mwisho ni kuwa Zoe ana interest sana na kusoma vitabu. Hii hobby ameniambukiza kidogo pia na inampa sana upeo wa kufanya vitu vingi hata creativity yake vitabu vimekuwa na nafasi kubwa sana. Hili swala la kusoma vitabu nitalileta kwenu kwa undani

Asante sana Zoe kwa kuniruhusu kueleza KUHUSU wewe. Kwako sky is the limit....Naamini nitaandika tena kuhusu wewe siku nyingine.

Stay tuned for more
Image result for zoe malaika glorious

ATM


Wednesday, June 24, 2015

For the love of fashion

Hello dear readers,

I believe the week is great to you, if not, I pray that it gets better.

One of the things that a lot of people do not know about me is that I LOVE fashion, and the reason that they do not know it is because I am not a fashionista. I don't know how that sounds but I will say I under dress most of the time and I don't put much effort when I dress up, should I change this? I really don't know but never say never. Hahahahahha.

So very soon I will introduce you to my fashion inspiration and my dear friend Zoe Glorious. She has been inspiring me for years on different things and I hope she will be an inspiration to you too.

Stay tuned.
IMG_0040
Much Love,

ATM