Habari,
Naamini wewe ni mzima. Samahani kwa kuwa kimya sana, ila mambo
yote ni mema.
Kwa kipindi cha kama miezi miwili nitaweka posts za watu ambao ni
ordinary na wanafanya mambo mazuri na wana-inspire wengi.
Leo naanza na Zoe Prudence Shoo
Nimemfahamu Zoe nikiwa Shinyanga Commercial Institute. Siku ya
kwanza nimefika shule (Tulikutana bafuni....hahahaha). Ndani ya dakika
chache urafiki ulizaliwa.
Nilisema mimi napenda fashion ila Zoe ni fashion Icon, yaani akiwa
mbele ya kioo is all fashion. Watu waliosoma Shycom wanaweza kukueleza jinsi Zoe alikuwa anapenda sana kupiga picha and she had her heart in all the pictures she took. Sisi tuliona ni ordinary pictures ila kwake it was a way of making her identity.
A fashion Icon.
Nilipomuuliza Zoe aniambie kuhusu yeye kwa kifupi aliniambia yeye
ni Creative, Zoe has the ability to think outside the box na kukupa jambo la
tofauti, haogopi kuthubutu na hilo ni jambo ambalo linamfanya yeye kuwa mtu wa
tofauti sana na kati ya watu ambao ningependa kufanya naye kazi huko baadae ni
yeye.
Nilipokuwa nawaza kuhusu Creativity ya Zoe niliwaza kuwa ili Zoe
aweze kuwa mtu creative ilihitaji kuwa na wazazi waelewa. Nimepata bahati ya
kukutana na mama yake na nilijua kwanini Zoe ni mtu wa tofauti sana.
Wazazi tuna nafasi ya muhimu sana ya jinsi watoto wetu wanavyoweza
kuja kuwa wanapokuwa watu wazima. Naamini kwenye kumruhusu mtoto kuwa na
imagination na kumtia moyo na sio kumkataza kila jambo, tunawawekea vikwazo katika kubuni
mambo kwenye maisha. Mtoto wangu ana potty ambayo inakuwa assembled upya kila
anapoitumia…alipoanza kutumia tulimpa nafasi ya kurudisha potty katika hali
yake ya mwanzo na ni jambo analo weza sana.
Jambo lingine ni kumruhusu kutumia
vyombo vyote, hata vinavyopasuka. Genesis hajafikisha miaka miwili ila anajua
kuwa chombo hiki ni delicate na kina hitaji extra care na kwa jinsi hiyo anakuwa
na confidence. Haya ni mambo madogo ila yanaweza kuleta impact kubwa kwa mtoto
Zoe ni mtu ambaye ana huruma na upendo wa ajabu, ni kati ya watu
jasiri sana niliowahi kukutana nao. Ni mtu mwenye sincere heart na nimekwambia
hapo juu kuwa nilipokutana na mama yake nilijua kwanini. Jinsi tunavyowapenda
watoto wetu na kuwalinda inawapa confidence katika jamii ila pia inawasaidia
kuwapa watu wengine the same amount of love they have received from us. Wapende
watoto wako sana it can change the world.
Jambo la muhimu sana la mwisho ni kuwa Zoe ana interest sana na kusoma vitabu. Hii hobby ameniambukiza kidogo pia na inampa sana upeo wa kufanya vitu vingi hata creativity yake vitabu vimekuwa na nafasi kubwa sana. Hili swala la kusoma vitabu nitalileta kwenu kwa undani
Asante sana Zoe kwa kuniruhusu kueleza KUHUSU wewe. Kwako sky is the limit....Naamini nitaandika tena kuhusu wewe siku nyingine.
Stay tuned for more
ATM